Home Habari Kuu Kampuni ya Lesedi yatakiwa kukabidhi mahakama hatimiliki

Kampuni ya Lesedi yatakiwa kukabidhi mahakama hatimiliki

0
Mahakama za Thika.

Mahakama moja ya Thika imeagiza  kampuni ya kuuza ardhi ya Lesedi kuikabidhi hatimiliki ya ardhi inayohusishwa na kesi ya ulaghai wa shilingi milioni tano ili kulinda haki za walalamishi wanaotaka fidia.

Hakimu Mkuu wa Thika Stella Atambo pia imemuagiza Martha Ndung’u ambaye ni mmiliki wa awali wa ardhi aliyouzia kampuni ya Lesedi, kuwasilisha stakabadhi za ardhi hiyo kwa ofisi ya usajili wa ardhi mjini Thika ili kusaidia katika kutolewa kwa hatimiliki mpya kabla ya Aprili 4, 2023.

Wakati huohuo, hakimu huyo alikataa kuondoa kibali cha kukamatwa kwa afisa mkuu mtendaji wa Lesedi Geofrey Kiragu baada ya kutofika mahakamani kwa kisingizio kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili unaosababishwa na msongo wa mawazo.

Atambo alisema kuwa ripoti ya matibabu iliyowasilishwa mahakamani lazima ithibitishwe kwanza na afisa anayefanya uchunguzi ili kubainisha iwapo ni halali.

Kiragu anakabiliwa na makosa 12 ya kupokea fedha kwa udanganyifu baada ya walamishi 12 kufika mahakamani wakitaka kufidiwa.

Wakili wake aliiambia mahakama kuwa mshukiwa ana mpango wa kuwafidia walalamishi hao kwani ameanza kuwagawanyia ardhi hiyo.

Kiragu aliuziwa shamba hilo na Njeri ila hakubadilisha umiliki wake.

Kutokana na hayo, mahakama hiyo iliwaita msajili wa ardhi eneo la Thika pamoja na Njeri kutoa mwanga kuhusiana na ardhi hiyo.

Njeri aliahidi kuwasilisha stakabadhi za ardhi hiyo ili hatimiliki mpya itolewe kwa jina la Lesedi Developers Ltd.

Kesi hiyo itaendelea Aprili 4, 2024.

Alphas Lagat
+ posts