Home Biashara Kampuni ya Bolt kuzindua magari ya umeme nchini Kenya

Kampuni ya Bolt kuzindua magari ya umeme nchini Kenya

Kampuni ya magari ya usafiri ya Bolt imetangaza kuwekeza kima cha shilingi milioni 100 kununua magari na pikipiki za kutumia umeme nchini Kenya.

0

Kampuni ya magari ya usafiri ya Bolt imetangaza kuwekeza kima cha shilingi milioni 100 kununua magari na pikipiki za kutumia umeme nchini Kenya.

Kampuni hiyo tayari inatumia zaidi ya pikipiki 40 za umeme zinazotumiwa kusafirisha bidhaa katika kuanti ya Nairobi.

Kulingana na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Bolt yenye makao makuu nchini Estonia,Martin Villig wanalenga kuondoa magari yanayotumia mafuta na badala yake kuwa na chaguo mbadala la magari ya umeme katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Bolt wamechukua hatua hiyo kama njia moja ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kupunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na matimizi ya magari yanayotumia mafuta.

Website | + posts