Home Michezo Kambi ya mazoezi kwa wanariadha chipukizi yaingia wiki ya mwisho

Kambi ya mazoezi kwa wanariadha chipukizi yaingia wiki ya mwisho

0
kra

Kambi ya mazoezi kwa wanariadha chipukizi wa Kenya imeingia juma la mwisho mapema Jumatatu, katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani .

Timu ya wanariadha 19 inajiandaa kwa mashindano ya Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, yatakayoandaliwa mjini Lima, Peru kati ya Agosti  27 na 31.

kra

Kulingana na mkurugenzi wa riadha ya chipukizi Barnaba Korir, wamejiandaa vyema kwa mashindano ya Dunia wakitarajia matokeo mazuri.

“Vijana wamejiandaa vizuri katika muda ambao wamekuwa kwenye kambi hapa Kasarani na wanatarajia kuondoka nchini mwishoni mwa juma hili.”akasema Korir

Kikosi cha Kenya kinachoongozwa na kocha Robert  Ng’isirei, kinawajumuisha bingwa wa Afrika katika mita 800 Sarah Moraa, na mshindi wa nishani ya fedha barani Afrika katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji  Edmund Serem ambao ni manahodha.

Kenya ilimaliza kwa nishani 10 katika makala ya mwaka 2022 mjini Cali,Colombia kwa dhahabu 3 fedha 3 na shaba 4.

Website | + posts