Home Kimataifa Kamati ya bunge yawasaili walioteuliwa kuwa Waziri wa EAC, Mwanasheria Mkuu

Kamati ya bunge yawasaili walioteuliwa kuwa Waziri wa EAC, Mwanasheria Mkuu

0
Beatrice Askul Moe aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Beatrice Askul Moe aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kra

Kamati ya bunge leo Ijumaa inawasaili watu wawili walioteuliwa kujiunga na Baraza Jipya la Mawaziri. 

Wa kwanza kufika mbele ya kamati ya usaili inayoongozwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula ni Beatrice Askul Moe aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Maendeleo ya Kikanda.

kra

Wadhifa huo awali ulishikiliwa na Peninah Malonza ambaye alipigwa kalamu wakati Rais William Ruto alipovunja Baraza la zamani la Mawaziri.

Aidha, Dorcas Oduor aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu anatarajiwa kufika mbele ya kamati hiyo leo Ijumaa kuanzia saa sita mchana ili kupigiwa msasa wa kubaini ikiwa anastahiki kuhudumu katika wadhifa huo.

Ikiwa uteuzi wake utaidhinishwa, Oduor atamrithi Justin Muturi aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Utumishi wa Umma na kuwa mwanamke wa kwanza nchini kuwahi kuhudumu katika wadhifa huo.

Kupigiwa msasa kwa wawili hao kunamaanisha kuwa amesalia mtu mmoja atakayefika mbele ya kamati hiyo ili kusailiwa.

Naye ni yule atayateuliwa kuwa Waziri wa Jinsia baada ya kamati hiyo kukataa uteuzi wa Stella Soi Lang’at kuhudumu katika wadhifa huo.

 

 

 

Website | + posts