Home Kimataifa Kamati ya bunge kuhusu maji yahoji matumizi yaliyopitiliza ya fedha katika idara...

Kamati ya bunge kuhusu maji yahoji matumizi yaliyopitiliza ya fedha katika idara ya maji

0
Kangogo Bowen, mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu maji
kra

Kamati ya bunge kuhusu Uchumi wa baharini, Maji na unyunyiziaji mashamba maji ikiongozwa na mwenyekiti Kangogo Bowen mbunge wa Marakwet Mashariki ilikutana na wawakilishi wa idara ya maji na usafi wa mazingira kujadili kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24.

Wakiongozwa na wawaziri wa maji Eric Mugaa na Katibu wa wizara hiyo Julius Korir, viongozi hao waliifahamisha kamati hiyo kuwa bajeti iliyotengwa ilikuwa na kiwango cha asilimia 90 cha matumizi ya mara kwa mara na asilimia 75 kwa matumizi ya maendeleo katika kipindi hicho.

kra

Bajeti iliyoidhinishwa ya 2023/2024 ilikuwa shilingi bilioni 50.37, ambapo bilioni 5.687 zilikuwa za kawaida na bilioni 44.68 za matumizi ya maendeleo.

Kati ya pesa hizo za matumizi zilikuwa bilioni 39.793, ambapo bilioni 5.107 zilikuwa za matumizi ya kawaida na bilioni 33.686 zikatumika kwa maendeleo kulingana na katibu Korir.

Hatua muhimu zilizopigwa mwaka huo wa kifedha ni pamoja na kuweka mipango, mifumo na taratibu za kufikia hatua kwa hatua upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwa wote kupitia afua za muda mfupi na mrefu, kwa kuongeza uwezo wa kuvuna na kuhifadhi maji, kujenga na kupanua mifumo ya maji taka na kuendeleza na kupanua mitandao ya usambazaji wa maji na usafi wa mazingira.

Wabunge walibaini tofauti kadhaa katika stakabadhi zilizowasilishwa na wizara kuhusu utekelezaji wa bajeti iliyotengwa mwaka wa 2023/24, huku mradi wa Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Kiambere-Mwingi ukitoa majibu tofauti kutoka kwa viongozi, kwa nini fedha zilizotengwa kwa mradi zimeelekezwa kwa mambo mengine na hali ya mradi ni ipi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo mheshimiwa Bowen pia alihoji matumizi makubwa ya fedha katika miradi mbalimbali, ambapo hadi sasa, miradi hiyo imepanda na zaidi ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

Katibu Julius Korir akijibu alisema kuwa kupunguzwa kwa bajeti wakati wa Nyongeza ya pili kuliathiri bajeti ambayo ilikuwa imefanywa kuhusiana na makadirio ya nyongeza ya kwanza.

Website | + posts