Home Kimataifa Kamanda mpya wa kitengo cha polisi cha idara ya mahakama akaribishwa

Kamanda mpya wa kitengo cha polisi cha idara ya mahakama akaribishwa

0
kra

Msajili mkuu wa idara ya mahakama Bi. Winfridah B. Mokaya jana katika majengo ya mahakama ya upeo nchini jijini Nairobi, alimpokea Ibrahim Ramadhan Omar, kamanda mpya wa kitengo cha polisi katika idara ya mahakama.

Wakati wa Omar alikuwa anakabidhiwa mamlaka na kamanda anayeondoka wa kitengo hicho Samuel Ndugu, msajili mkuu wa idara ya mahakama alimfahamisha kuhusu mahitaji ya ulinzi katika idara hiyo.

kra

Mahitaji hayo ni pamoja na ulinzi kwa majaji na maafisa wote wa idara hiyo pamoja na ulinzi wa majengo na vifaa vingine vya idara hiyo kote nchini.

Ibrahim Ramadhan Omar ana tajriba ya miaka 36 katika huduma ya taifa ya polisi, jukumu la hivi punde zaidi likiwa katika kitengo cha ulinzi wa majengo ya serikali na viongozi mashuhuri serikalini.

Mokaya alimtaka kamanda huyo mpya kutoa kipaumbele kwa shughuli ya kuongeza maafisa zaidi wa polisi katika kitengo hicho cha polisi cha idara ya mahakama.

Alisisitiza haja iliyopo ya kuhamasisha maafisa wote wa idara ya mahakama kuhusu mifumo ya ulinzi wa kibinafsi kila mara.

Kitengo cha polisi wa idara ya mahakama kilibuniwa mwaka 2021 baada ya mashauriano kati ya jaji mkuu Martha Koome na Inspekta Jenerali wa polisi wa wakati huo Hillary Mutyambai.

Website | + posts