Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka anasema na liwe liwalo, hatajiunga na serikali ya Kenya Kwanza.
Kumekuwa na uvumi kwamba Kalonzo huenda akajiunga na serikali hiyo, huku wengi wakikisia kuwa huenda akateuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu.
“Wanadhani mimi Kalonzo wa Musyoka, naweza kuingia serikali ya aina hiyo?” Alisema Kalonzo wakati akifutilia mbali uvumi huo leo Ijumaa akiwa huko Nyeri.
Matamshi yake yanakuja wakati baadhi ya wanachama wa ODM, ambacho ni chama tanzu cha muungano wa Azimio, wameteuliwa kuwa Mawaziri katika utawala wa Kenya Kwanza.
Wao ni pamoja na John Mbadi, Opiyo Wandayi, Hassan Ali Joho na Wycliffe Oparanya.
Hatua hiyo imesababisha migawanyiko mikubwa katika muungano wa Azimio huku chama cha NARC Kenya kikianza mchakato wa kuugura muungano huo.