Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka amekosoa bajeti ya mwaka huu akisema haina ukweli.
Akiongea katika kaunti ya Taita Taveta, makamu huyo wa rais wa zamani, alisema mapendekezo mapya ya ushuru ni kinyume cha katiba na yatawasababishia wakenya mateso.
Kalonzo alisema hakuna nchi yoyote ambayo imepiga hatua za maendeleo kupitia kuwatoza raia wake ushuru kupitia kiasi.
Aidha, alitoa wito kwa serikali kubatilisha sera yake ya ushuru akisema itawaongezea wakenya mzigo.
Kalonzo wakati huo huo aliwapongeza wabunge wa muungano wa Azimio la Umoja kwa kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2023.