Home Michezo Kales na Jepkosgei watwaa ubingwa wa Ol’Bolossat Half Marathon

Kales na Jepkosgei watwaa ubingwa wa Ol’Bolossat Half Marathon

0

Enos Kales wa Kapenguria na Winnie Jepkosgei kutoka Elgeyo Marakwet ndio mabingwa wa makala ya kwanza ya mbio za Lake Ol’Bolossat Half Marathon zilizoandaliwa Jumapili kaunti ya Nyandarua .
 
Kales alikata utepe kwa saa 1 dakika 6 na sekunde 15, akifuatwa na Amos Mitei kwa sa 1 dakika 6 na sekunde 43, huku Nicholas Kiplimo, akimaliza wa tatu .

Jepkosgei alishinda mbio za vipusa kwa saa 1 dakika 14 na sekunde 39 mbele ya Vivian Jerotich, aliyechukua nafasi ya pili kwa saa 1 dakika 14 na sekunde 55, naye Beatrice Chepkemoi akaridhia nafasi ya tatu.

Kales na Jepkosgei walituzwa shilingi laki mbili kila mmoja, huku waliomaliza katika nafasi za pili wakitunukiwa shilingi 150,000 na shilingi laki moja kwa waliomaliza wa tatu.

Samuel Njihia na Faith Chepkoech waliibuka washindi wa kilomita 10.