Home Habari Kuu Kalenda ya masomo mwaka 2024 yatolewa

Kalenda ya masomo mwaka 2024 yatolewa

0
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu
Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu

Shule za chekechea, msingi na sekondari zitafunguliwa Januari 4, 2024 na masomo kuendelea kwa kipindi cha wiki 13. 

Wizara ya Elimu inasema shule hizo zitafungwa Aprili 5, 2024.

Shule hizo zitanatarajiwa kufungwa mwishoni mwa mwezi huu ili kupisha kipindi cha mitihani ya KCPE, KPSEA na KCSE.

Kwa mujibu wa kalenda ya masomo iliyotolewa na Wizara ya Elimu leo Ijumaa,  katika muhula wa kwanza, wanafunzi wataenda mapumzikoni ya katikati ya muhula kati ya Februari 29 na Machi 3, 2024.

Muhula wa pili utaanza Aprili 29 hadi Agosti 2, 2024 wakati wanafunzi wakienda kwenye mapumziko ya katikati ya muhula kati ya Juni 20 na Juni 23, 2024.

Muhula wa tatu utang’oa nanga Agosti 26, 2024 na kuendelea hadi Oktoba 25, 2024 na kama kawaida, muhula huo hautakuwa na kipindi cha mapumziko ya katikati ya muhula kutokana na ufupi wake.

Mitihani ya kitaifa itafanywa kati ya Oktoba 28 na Novemba 22, 2024.

Kwa upande wa vyuo vya mafunzo ya walimu, muhula wa kwanza utaanza Januari 8, 2024 na kumalizika Aprili 5, 2024 wakati ule wa pili ukianza Aprili 29 na kumalizika Agosti 2, 2024.

Kipenga cha muhula wa tatu kitapulizwa Agosti 26 na kumalizika Novemba 8, 2024.

Website | + posts