Home Biashara Kahawa: Gachagua asema wamejifunza mengi kutoka kwa Colombia

Kahawa: Gachagua asema wamejifunza mengi kutoka kwa Colombia

0

Naibu Rais Rigathi Gachagua anasema wamejifunza mengi kutoka kwa Colombia kuhusiana na masuala yanayofungamana na kilimo cha kahawa.

Gachagua anaongoza ujumbe unaojumuisha Mawaziri Mithika Linturi wa Kilimo na Dkt. Alfred Mutua wa Mambo ya Nje pamoja na wakulima kwa ziara ya siku nne nchini Colombia ili kujifunza mbinu bora za kilimo cha kahawa na uongezaji thamani.

Colombia ni nchi inayoongoza katika uzalishaji wa kahawa duniani. Inazalisha na kuuza kahawa katika mataifa kama vile Marekani, Ujerumani na Ubelgiji, masoko ambayo Kenya inayalenga kupitia kuiongezea kahawa thamani.

“Tumejifunza mengi shambani kutoka kwa uzalishaji hadi utekelezaji sera. Hatua kadhaa tunazotekeleza zimeboreshwa; sasa tuna njia bayana na yenye uelewa ya namna ya kuweka pesa katika mfuko wa mkulima,” alisema Gachagua akiwa ameandamana na mwenyeji wake Francia Elena Márquez Mina ambaye ni Makamu wa Rais wa Colombia.

“Tuna dhamira ya kutekeleza mabadiliko na Mpango, huku siku bora zikikaribia.”

Utawala wa Kenya Kwanza umeahidi kuifanyia mabadiliko makubwa sekta ya kahawa nchini na kukabiliana na matapeli ambao wamekuwa wakivuna wasikopanda wakati wakulima wa kahawa wakihangaika kwa miaka mingi iliyopita.

Website | + posts