Rais William Ruto mapema Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi ameongoza kuapishwa kwa Mkuu mpya wa Majeshi Jenerali Charles Muriu Kahariri.
Wengine waliokula kiapo ni Jenerali John Omenda ambaye atakuwa naibu Mkuu wa Majeshi ,Fatuma Ahmed ambaye ni Kamanda wa jeshi la hewa na Brigedia Paul Otieno aliyepandishwa hadhi hadi wadhfa wa Meja Jenerali wa jeshi la wanamaji.