Home Habari Kuu Kagame aidhinishwa kuwania Urais kwa muhula mwingine

Kagame aidhinishwa kuwania Urais kwa muhula mwingine

0

Chama tawala nchini Rwanda kimemwidhinisha Rais Paul Kagame kuwania Urais kwa muhula mwingine kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwandaliwa Julai mwaka huu.

Endapo atachaguliwa Kagame atahudumu kwa takriban miaka 30 tangu atwae mamlaka mwaka 2000.

Kagame alipendekezwa na asilimia 99.1 ya wanachama wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF) .

Rais Kagame alishinda muhula wa pili mwaka 2017 akipata asilimia 98.6 ya kura kulingana na tume ya uchaguzi .

Rwanda ilibadilisha katiba mwaka 2015 inayomaanisha Kagame anaweza kuwania Urais kwa mihula miwili ya miaka mitano kila moja baada ya mwaka huu.

Website | + posts