Home Michezo Juventus yafurushwa Europa Conference league kwa utundu

Juventus yafurushwa Europa Conference league kwa utundu

Juve maarufu kama Old Lady wametozwa haka ya pauni milioni 17 nukta 14, wakati Chelsea wakipigwa faini ya pauni milioni 8 nukta 57.

0

Juventus imeng’atuliwa kuahiriki mashindano ya kuwania kombe la UEFA Europa Conference League msimu ujao kwa ukiukaji wa sheria A fedha FFP.

UEFA pia imeitoza faini Juventus na Chelsea kwa kukiuka sheria za fedha na kutoa taarifa za fedha zisizo kamilifu.

Kulingana na shirikisho la soka ulaya Juventus imepatikana na hatia ya kukiuka sheria za fedha ilipowasajili wachezaji kati ya mwaka 2012 na 2019 .

Juve maarufu kama Old Lady wametozwa haka ya pauni milioni 17 nukta 14, wakati Chelsea wakipigwa faini ya pauni milioni 8 nukta 57.

Shirikisho la soka nchini Italia linapaswa kuteua timu nyingine itakayochukua nafasi ya Juventus katika kipute cha Conference League msimu ujao.

Juve imesema haitakata rufaa uamuzi huo.

Website | + posts