Justice Antony Mrima, amechaguliwa kuwa mwanachama wa tume ya kuwaajiri wahudumu wa idara ya mahakama nchini, JSC.
Sasa Jaji huyo sasa atawakilisha chama cha Majaji na Mahakimu (KMJA), kuambatana na sehemu ya 171 (2)(d) ya katiba.
Justice Mrima aliwapiku washindani wake kwa kuzoa kura 95, na kuwashinda Justices Sila Munyao na James Olola, waliopata kura 27 na 15 mtawalia.
“Chama cha Mahakimu na Majaji kimemchagua Justice Antony Mrima kuwa mwakilish wake wa kiume katika tume ya kuwaajiri wafanyakazi wa idara ya mahakama,” ilisema tume ya JSC kupitia mtandao wa X.
Justice Mrima, anachukua mahala pa marehemu Jaji David Majanja, aliyefariki mwezi Julai,2024 akipokea matibabu hospitalini.