Home Habari Kuu Jumla ya watu 238 wamefariki kutokana na mafuriko hapa nchini

Jumla ya watu 238 wamefariki kutokana na mafuriko hapa nchini

Kaunti za Makueni, Nyandarua, Nakuru na Bomet pia zimeathiriwa na maporomoko ya ardhi.

0
Hatibu wa serikali Isaac Mwaura, akizungumza na wanahabari.

Idadi jumla ya watu 238 wamefariki hapa nchini, kutokana na mvua inayonyesha na ambayo imesababisha mafuriko.

Hatibu wa serikali Isaac Mwaura leo Jumanne, alitangaza kwamba watu 75 wameripotiwa kupotea huku familia 47,000 zikiachwa bila makao.

Miongoni mwa kaunti zilizoathiriwa, kaunti ya Nairobi inaongoza huku idadi ya waathiriwa ikiwa ni 164,000.

Kaunti za Makueni, Nyandarua, Nakuru na Bomet pia zimeathiriwa na maporomoko ya ardhi.

Mwaura alisema kumekuwa na uharibifu wa mali, miundomsingi pamoja na vifo vya mifugo hali hii ikiacha wengi wakikadiria hasara kwenye maeneo mengi nchini.

Kwa mujibu wa agizo la serikali kuhusu kufunguliwa kwa shule, Mwaura alifichua kuwa takriban wanafunzi laki sita watatatizika kimasomo kwa kuwa shule zao zinatumika kama makazi ya muda kwa waliopoteza makao.

Vyoo vingi vya shule vimefurika maji na mapaa yamepeperushwa na upepo.

Website | + posts