Home Habari Kuu JSC yatangaza nafasi 11 za majaji wa Mahakama ya Rufaa

JSC yatangaza nafasi 11 za majaji wa Mahakama ya Rufaa

Hatua hiyo inafuatia mkutano wa mwezi jana baina ya viongozi wa nguzo tatu za serikali katika ikulu ya rais.

0

Tume ya kuwaajiri maafisa wa idara ya mahakama, JSC imetangaza nafasi 11 za majaji wa mahakama ya rufaa.

Kupitia gazeti rasmi la serikali, Jaji Mkuu Martha Koome aliwataka Wakenya waliohitimu kwa nyadhifa hizo kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya JSC.

Hatua hiyo inafuatia mkutano wa mwezi jana baina ya viongozi wa nguzo tatu za serikali katika ikulu ya rais.

Wakati wa mkutano huo, Rais Ruto aliahidi nyogeza ya bajeti kwa idara ya mahakama kuiwezesha kuwaajiri majaji 36 zaidi, 11 kati yao wakiwa majaji wa mahakama ya rufaa huku wengine wakiwa majaji wa mahakama kuu.

Idara ya mahakama aidha ilipata nyongeza ya pesa kwa matumizi ya shughuli za uchukuzi.

Idara hiyo itapokea pesa za kukodisha magari ya kutumiwa na maafisa wake.

Website | + posts