Home Habari Kuu Atwoli, wengine 6 wateuliwa kwenye jopo la kumtafuta mrithi wa Noordin Haji

Atwoli, wengine 6 wateuliwa kwenye jopo la kumtafuta mrithi wa Noordin Haji

0

Rais William Ruto ameteua jopo la uteuzi la watu saba litakaloongoza mchakato wa kumtafuta mrithi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji.

Haji kwa sasa anahudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Ujasusi Nchini, NIS baada ya kuapishwa katika Ikulu ya Nairobi Juni 14, 2023.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Nchini, COTU Francis Atwoli na Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadamu Roseline Odede ni miongoni mwa wanachama wa jopo hilo.

Wengine ni Wakili Mkuu wa serikali Shadrack Mose na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Kupambana na Ufisadi Nchini (EACC) Twalib Abdallah Mbarak.

Mary Kimonye, Mary Adhiambo Maungu na Richard Onsongo Obwocha pia wameteuliwa na Rais kuwa wanachama wa jopo hilo.

Jopo hilo linatarajiwa kuwapigia msasa watakaotuma maombi ya kutaka kumrithi Haji na kisha kupendekeza majina matatu kwa Rais.

Kisha Rais atateua jina moja kati ya hayo atakalolituma bungeni ili aliyeteuliwa apigwe msasa na wabunge.

Ikiwa uteuzi huo utaidhinishwa, jina lake litarejeshwa kwa Rais ili kuteuliwa rasmi kwa wadhifa huo.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here