Home Biashara Joho: Nitaboresha uchimbaji Madini na Uchumi wa Baharini

Joho: Nitaboresha uchimbaji Madini na Uchumi wa Baharini

Na ili kuhakikisha malengo ya wizara hiyo yanatimizwa, Joho alisema atapiga jeki uwekezaji katika viwango vyote, ili Wakenya wanufaike kutokana na shughuli za wizara hiyo.

0
Waziri wa Biashara Salim Mvurya (Kushoto), Na mwenzake wa Uchumi wa Baharini Hassan Joho.
kra

Waziri mpya wa Madini na Uchumi wa Baharini Hassan Ali Joho, amewahakikishia Wakenya kujitolea kwake kutumia ujuzi na tajriba yake kuifanya wizara yake kuwa kichocheo kikuu ch uchumi kufanikisha ajenda ya maendeleo ya taifa hili.

“Nitashirikiana kwa karibu na wenzangu katika wizara hii pamoja na mawaziri wenzangu kuhakikisha ruwaza ya kubuni nafasi za ajira katika wizara hii inafanikiwa,” alisema waziri huyo.

kra

Waziri huyo aliyasema hayo Jana Ijumaa katika makao makuu ya wizara hiyo Jijini Nairobi, alipokabidhiwa rasmi wizara hiyo na mtangulizi wake Salim Mvurya, ambaye sasa ni waziri wa biashara, uwekezaji na viwanda.

Na ili kuhakikisha malengo ya wizara hiyo yanatimizwa, Joho alisema atapiga jeki uwekezaji katika viwango vyote, ili Wakenya wanufaike kutokana na shughuli za wizara hiyo.

“Tunataka wawekezaji wawekeze hapa nchini katika uchumi wa baharini, madini na shughuli za baharini. Mojawepo wa lengo letu kuu ni uongezaji dhamani,” alisema waziri Joho.

Kwa upande wake, waziri  Mvurya, alimshukuru Rais Ruto kwa kumteua yeye pamoja na Joho kuhudumu katika nyadhifa hizo, akisema wizara ya biashara itashikiriana na ile ya madini kuikuza uwekezaji nchini.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na makatibu wa wizara Betsy Njagi (Uchumi wa baharini na uvuvi) na Geoffrey Kaituko (Shughuli za baharini na safari za meli). Wengine pia waliohudhuria ni maafisa wa ngazi za juu katika wizara hizo.

Website | + posts