Home Kimataifa Jiji la Khartoum laghubikwa na maambukizi ya ukambi

Jiji la Khartoum laghubikwa na maambukizi ya ukambi

0

Kumekuwa na ongezeko la visa vya ugonjwa wa ukambi katika mji mkuu wa Khartoum nchini Sudan.

Visa hivyo vimechochewa na mzozo unaoendelea jijini humo, ambao unatatiza juhudi za utoaji wa chanjo kwa mujibu wa daktari mmoja wa watoto.

Akiongea na mpango wa Sudan Lifeline, Dkt. Mohamed al-Taher anayefanya kazi mjini Khartoum, alisema kuna upungufu wa chanjo ambao huenda ukasababisha ongezeko la maambukizi miongoni mwa watoto.

Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka la Medecins Sans Frontieres, limeonya kwamba kuna ongezeko la visa vya ugonjwa wa ukambi na utapia mlo kwenye kambi za wakimbizi zilizo katika jimbo la White Nile, kusini mwa Khartoum.

Shirika hilo limesema jamii zimeripoti ongezeko la vifo vya watoto vinavyoshukiwa kusababishwa na ukambi.

Jeshi la nchi hiyo na kikosi cha dharura RSF, zinakabiliana kudhibiti Jiji kuu la Khartoum, vita ambavyo vimesababisha maafa na kuwaacha wengi bila makao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here