Home Habari Kuu Jiandaeni kwa mvua kubwa hadi Januari, Wakenya waonywa

Jiandaeni kwa mvua kubwa hadi Januari, Wakenya waonywa

0

Wakenya wametahadharishwa kujiandaa kwa mvua kubwa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo hadi mwezi Januari mwakani.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema maeneo mengi nchini yataendelea kupokea viwango vya juu vya mvua, mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Maeneo ya bonde la ufa, Ziwa Victoria, Nyanza, magharibi ya nchi na mashariki yamekuwa yakishuhudia mvua kubwa tangu katikati ya mwezi uliopita.

Mvua hiyo imesababisha uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo huku watu kadhaa wakiripotiwa kufariki kutokana na athari za mafuriko.

Kunao walioripotiwa kujeruhiwa kutokana na mafuriko ambayo pia yamesababisha barabara kadhaa kuharibika na kutopitika.

Ni hali ambayo imesababisha viongozi katika kaunti ya Mandera kuitaka serikali kuu kuingilia kati kwa kutoa rasilimali muhimu zinazohitajika kukabiiliana na athari za mvua hizo.

 

Website | + posts