Home Habari Kuu Jeshi la Sudan lashambulia Mji Mkuu Khartoum

Jeshi la Sudan lashambulia Mji Mkuu Khartoum

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika mashambulizi hayo, huku 14 wakijeruhiwa na wanapokea matibabu.

0
kra

Jeshi la Sudan limeshambulia Mji Mkuu Khartoum, likilenga kutwaa eneo ambalo linashikiliwa na wapiganaji wa Rapid Support Forces (RSF).

Jeshi hilo lilitekeleza mashambulizi ya angani siku ya Alhamisi, dhidi ya maeneo yanayokaliwa na wapiganaji wa RSF, ikiwa ni pamoja na Khartoum kaskazini.

kra

Kulingana na duru nchini humo, jeshi la Sudan sasa linadhibiti madara matatu, yanayojumuisha mawili yanayounganisha mji wa Omdurman na Khartoum.

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika mashambulizi hayo, huku 14 wakijeruhiwa na wanapokea matibabu.

Mashambulizi hayo yalilenga makazi ya raia kaskazini mwa mji wa Omdurman, kulingana na msemaji wa wizara ya afya ya Khartoum Mohamed Ibrahim.

Ibrahim alisema waliojeruhiwa wanapokea matitabu katika hospitali ya Al-No.

Website | + posts