Home Habari Kuu Jeshi la Israel limedai kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah

Jeshi la Israel limedai kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah

Hata hivyo kundi la Hezbollah halijatoa habari za kuthibitisha kuuawa kwa kiongozi wake.

0
Israel yadai kumuua kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah.
kra

Jeshi la Israel IDF, leo Jumamosi limesema kiongozi wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah, aliuawa katika shambuli la Israel lililotekelezwa Beirut,siku ya Ijumaa.

“Hassan Nasrallah amefariki,” msemaji wa IDF Luteni kanali Nadav Shoshani alitangaza kupitia mtandao wa X.

kra

Captain David Avraham, ambaye pia ni msemaji wa jeshi hilo, alithibitishia shirika la habari la AFP kuwa kiongozi huyo wa Hezbollah ameuawa, kufuatia mashambulizi ya Israel siku ya Ijumaa.

Hata hivyo kundi la Hezbollah halijatoa habari za kuthibitisha kuuawa kwa kiongozi wake.

Kulingana na taarifa za jeshi la Israel, mashambulizi hayo pia yalisababisha kifo cha Ali Karake, ambaye ni kamanda wa Hezbollah katika eneo la kusini pamoja na idadi isiyojulikana ya makamanda wa kundi hilo.

Israeli imemshtumu Hassan Nasrallah kwa kutekeleza mauaji ya raia na wanajeshi wengi wa Israel, pamoja na kupanga na kutekeleza shughuli za kigaidi, alipokuwa Katibu Mkuu wa Hezbollah kwa muda wa miaka 32.

Hezbollah ilianza kuishambulia Israel siku moja baada ya kundi la Hamas kuivamia Israel Oktoba 7, 2023, hatua iliyosababisha vita kuzuka katika eneo la Gaza.

Israel katika siku za hivi karibuni imeelekeza mashambulizi yake Lebanon kutoka Gaza, ambapo mashambulizi makubwa ya mabomu yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 700 na wengine 118,000 wakiachwa bila makao.

Website | + posts