Home Habari Kuu Jeshi la Israel lasema linafanya ‘mashambulizi sahihi’ mjini Beirut

Jeshi la Israel lasema linafanya ‘mashambulizi sahihi’ mjini Beirut

0
Picha kwa hisani ya Al Jazeera
kra

Jeshi la Israel (IDF) limesema linafanya “mashambulizi sahihi” mjini Beirut nchini Lebabon. 

Hii ni licha ya wito unaoongozwa na Marekani wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Hezbollah.

kra

“IDF kwa sasa inafanya mashambulizi sahihi mjini Beirut. Maelezo ya kina kufuata,” limesema jeshi hilo katika taarifa.

Hayo yanajiri wakati shambulizi la Israel katika viunga vya kusini mwa mji wa Beirut leo Alhamisi lilimlenga kamanda wa Hezbollah, kwa mujibu wa chanzo cha habari kilichopo karibu na kundi hilo.

“Shambulizi la Israel lilimlenga kamanda wa Hezbollah,” chanzo hicho kilisema kikiomba kutotambuliwa kwani hawajaruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.

Hilo ni shambulizi la nne linalowalennga makamanda wa Hezbollah katika ene hilo katika kipindi cha wiki moja.

Website | + posts