Home Michezo Jepchirchir avunja rekodi ya dunia akitwaa ubingwa wa London Marathon huku Munyao...

Jepchirchir avunja rekodi ya dunia akitwaa ubingwa wa London Marathon huku Munyao akihakikisha ushindi maradufu kwa Wakenya

0

Bingwa wa Olimpiki Peres Jepchirchir ametwaa ubingwa wa makala ya mwaka huu ya mbio za London Marathon, huku akivunja rekodi ya dunia ya wanawake pekee wakati Alexander Mutiso Munyao akishinda mbio za wanaume .

Jepchirchir amevunja rekodi ya dunia ya wanawake pekee ya saa 2 na dakika 17 iliyokuwa ikishikiliwa kwa pamoja na bingwa wa London marathon Joyciline Jepkosgei na Megertu Alemu wa Ethiopia aliyemaliza pili mwaka jana.

Tigist Assefa wa Etahiopia amemaliza wa pili kwa saa 2 dakika 16 na sekunde 16 huku Joyceline Jepkosgei  akimaliza wa tatu kwa saa 2 dakika 16 na sekunde 24.

Wakenya wengine Brigid Kosgei na Sheila Chepkurui walichukua nafasi za 5 an 6 mtawalia huku 5th Ruth Chepng’etich akiridhia nafasi ya 10 .

Munyao alimbwaga Kenenisa Bekele kutoka Ethiopia na kushinda mbio za wanaume kwa saa 2 dakika 4 na sekunde 1,akifuatwa na Bekele kwa saa 2 na dakika 4 na sekunde 15 wakati Mwingereza Emile Cairess akiambulia nafasi ya tatu.

Website | + posts