Home Kimataifa Je, Oparanya afaa kwa Wizara ya Vyama vya Ushirika?

Je, Oparanya afaa kwa Wizara ya Vyama vya Ushirika?

Wadhani kuwa Oparanya anafaa zaidi katika wizara ya vyama vya ushirika au ile ya fedha?

0
Aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya.
kra

Kamati maalum ya Bunge la Kitaifa itaanza kuwasaili Mawaziri wateule kati ya Agosti 1 na 4 katika majengo ya bunge.

Kamati hiyo itaongozwa na Spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula

kra

Miongoni mwa walioratibiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni Gavana wa zamani wa Kakamega Wycliffe Oparanya.

Oparanya aliye na  umri wa miaka 68,  ni miongoni mwa kundi la Mawaziri wateule, walioratibiwa kusailiwa katika siku ya mwisho Agosti nne.

Oparanya ameteuliwa kuwa Waziri wa Vyama vya Ushirika na Mashirika Madogo na ya Kadiri ya Ujasiriamali nchin,i yaani MSME.

Oparanya ni mwanasiasa wa Kenya aliyehudumu katika wadhfa wa Gavana wa Kakamega, kwa mihula miwili hadi mwaka 2022.

Awali, alihudumu kama waziri wa maendeleo na mipango ya serikali na ruwaza ya mwaka 2030, katika serikali ya marehemu Rais Mwai Kibaki.

Kwa sasa, Oparanya ni naibu mwenyekiti wa chama cha ODM, kwa pamoja na aliyekuwa Gavana wa Moambasa Hassan Joho.

Oparanya ana tajriba ya miaka 23 katika maswala ya  usimamizi wa fedha humu nchini na kimataifa na pia uhasibu.

Pia ana shahada ya uzamifu katika uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dares es Salaam, Tanzania.

Umma una hadi Agosti Mosi kuwapiga msasa Mawaziri hao na kuwasilisha ripoti kwa kamati hiyo ya bunge.