Home Kimataifa Japani huenda ikamwaga baharini maji kutoka mtambo wa Fukushima hivi karibuni

Japani huenda ikamwaga baharini maji kutoka mtambo wa Fukushima hivi karibuni

0

Serikali ya Japani huenda hivi karibuni ikaanza kumwaga katika bahari ya Pasifiki maji yaliyotibiwa na kuzimuliwa ambayo bado yana mionzi kutoka kwenye mtambo wa nyuklia ulioharibika wa Fukushima Namba Moja. Hii ni baada ya shirika la Umoja wa Mataifa, UN la kushughulikia kawi ya nyuklia kuikubalia kufanya hivyo.

Ripoti zinaashiria kwamba maafisa wa serikali ya Japani watajukumiwa kuelezea mpango huo kwa wananchi walio karibu na nchi jirani huku kukiwa na hofu ya athari mbaya.

Maji hayo kwa sasa yamehifadhiwa kwenye matangi makubwa yapatayo 1,000 katika eneo palipo mtambo huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA Rafael Grossi alisema kwamba uchunguzi wa shirika hilo kuhusu mpango mzima wa kumwaga maji hayo umebaini kwamba unaambatana na kanuni za kimataifa za usalama. Alisema pia kwamba kumwagwa kwa maji hayo yaliyotibiwa taratibu na wala sio yote mara moja hadi baharini kutakuwa na athari ndogo sana ya mionzi kwa binadamu na mazingira.

Grossi anatarajiwa kuzuru eneo la Fukushima Jumatano akiwa na Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida.

Maji tani milioni 1.3, kiwango ambacho kinaweza kujaza vidimbwi 500 vya kuogelea vya michezo ya Olimpiki, yamekuwa yakiongezeka katika mtambo huo tangu Machi, 2011 wakati kilipoharibiwa na tsunami.

Mifumo ya umeme na ya kupoza iliharibiwa kabisa na kusababisha janga kubwa zaidi la kinyuklia.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here