Home Kimataifa Jamii za Ogiek na Endorois zapinga kufurushwa kutoka msitu wa Mau

Jamii za Ogiek na Endorois zapinga kufurushwa kutoka msitu wa Mau

Jamii hizo zilisema maisha yao yanavurugwa mara kwa mara na hatua hiyo, ikiwa ni pamoja na masomo ya watoto wao.

Jamii za Ogiek na Endorois zaandamana Jijini Nairobi.
kra

Jamii za Ogiek na Endorois zimetoa wito kwa serikali kukomeshe shughuli inayoendelea ya kuzifurusha kutoka msitu wa Mau, na badala yake kutekeleza maamuzi mawili ya mahakama ya Afrika ya kutetea haki za binadamu.

Wakati wa matembezi ya amani jijini Nairobi ya kuwasilisha malalamiko yao kwa mwanasheria mkuu, jamii hizo zilisema maisha yao yanavurugwa mara kwa mara na hatua hiyo, ikiwa ni pamoja na masomo ya watoto wao.

kra

Jamii ya Ogiek ilidokeza kuwa tume ya ardhi nchini ilipozuru ardhi yao, ilitoa ahadi kwamba itashughulikia maswala tata yaliyopo, lakini imesikitishwa kugundua kwamba imelaumiwa kwa kuharibu msitu wa Mau, madai ambayo jamii hiyo imeyapinga.

Daniel Kobei, mmoja wa wazee wa jamii ya Ogiek waliihimiza serikali badala yake kushauriana nao kuhusu baadhi ya mipango yake ukiwemo ule mpango wa mkopo wa kukabiliana na athari za hewa ya carbon.

Mnamo mwaka 2022, mahakama iliamrisha Kenya kuipa jamii hiyo hati ya pamoja ya ardhi ya mababu wao katika msitu wa Mau na kuilipa shilling million 157.85 kama fidia .

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts