Home Habari Kuu Jamii ya Wapemba yapewa uraia Kenya

Jamii ya Wapemba yapewa uraia Kenya

Idadi kubwa ya Wapemba inapatikana maeneo ya Kwale,Kilifi na Mombasa huku weachache wakizagaa Nakuru,Homabay na Kisumu.

0

Wapemba zaidi ya laki moja wanaoishi nchini wamepewa uraia kuwa mojawapo ya makabila ya Kenya.

Wapemba wamekuwa wakiishi nchini kwa miongo kadhaa ila hawajapewa kibali na kutabuliwa kuwa Wakenya kisheria huku idadi ndogo ya watu wapatao 7,000 wakisajiliwa.

Wapemba sasa wako huru kuwa na kitambulisho cha kitaifa na stakabadhi nyinginezo.

Idadi kubwa ya Wapemba inapatikana maeneo ya Kwale, Kilifi na Mombasa huku wachache wakizagaa Nakuru, Homabay na Kisumu.

Jamii hii ni maarufu kwa uvuvi, upigaji mbizi na kuendesha mashua .

Asili ya Wapemba ni kisiwani Zanzibar nchini Tanzania na waliingia nchini Kenya nyakati za Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here