Home Vipindi Jamii ya Sengwer yataka kukomeshwa kwa mipango ya kuwafurusha msituni Embobut

Jamii ya Sengwer yataka kukomeshwa kwa mipango ya kuwafurusha msituni Embobut

0
kra

Jamii ya Sengwer ambayo inaishi katika msitu wa Embobut kaunti ya Elgeyo Marakwet inataka suluhisho mwafaka liafikiwe kuhusu mustakabali wao.

Watu wa jamii hiyo wanahisi kwamba hilo litakuwa bora kuliko hatua ya wafanyakazi wa huduma za misitu nchini KFS ya kuchoma nyumba zao na kuwafurusha kila mara.

kra

Kulingana nao, agizo lililotolewa na mahakama linatosha kuwawezesha kuendelea kuishi katika eneo hilo la msitu kwani wana sheria zao kama jamii za kuishi kwenye msitu huku wakiutunza.

Shule zinapofunguliwa kwa muhula wa pili, wakazi hao wa Embobut wabahisi kwamba wanao watashindwa kwenda shuleni kwa sababu familia nyingi hujificha kwenye msitu kwa kuhofia maafisa wa KFS na kuchomwa kila mara kwa nyumba zao.

Elias Kimayo mmoja wa wakazi wa Embobut anaelezea kwamba watu wa jamii yao ya Sengwer wamekuwa wakiishi kwenye msitu huo tangu jadi lakini kuanzia miaka ya 1980 wamekuwa wakifurushwa.

Mama Eunice Paul alilalamika kwamba alichomewa nyumba pamoja na kila kitu kilichokuwa ndani akishangaa iwapo wao ni raia wa Kenya au wa nchi nyingine huku akiitaka serikali iwapeleke kwenye nchi hiyo badala ya madhila wanayopitia.

David Yator aliitaka serikali iafikie mapatano na watu wa jamii ya Sengwer ili kuhakikisha wanaishi katika eneo moja na wanatunza msitu huo.