Home Habari Kuu Jamii ya kimataifa yahimizwa kukabiliana na changamoto dhidi ya maendeleo endelevu

Jamii ya kimataifa yahimizwa kukabiliana na changamoto dhidi ya maendeleo endelevu

Ruto alitoa wito wa mageuzi katika mfumo wa ufadhili wa kimataifa hasa namna ya ulipaji madeni pamoja na ustawishaji wa taasisi za fedha za kimataifa.

0

Rais William Ruto ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuelekeza rasilimali katika juhudi za kukabiliana na changamoto dhidi ya malengo ya maendeleo endelevu.

Rais Ruto alisema kuwianisha mtaji wa kimataifa na malengo ya maendeleo endelevu, ni muhimu kwa ustawi unaozingatia hali ya anga.

Rais alisema kuwa mataifa mengi barani Afrika, yameshindwa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu kutokana na vizingiti kama vile madeni, mfumko wa bei, athari za mabadiliko ya tabia nchi na mizozo.

“Kwa kuimarisha uwezo wa Afrika kupata ufadhili kutoka hazina ya kimaendeleo duniani, tutafungua uwezo wa Afrika, rasilimali zake, ardhi ya kilimo na nguvukazi ya raia wake,” alisema kiongozi wa taifa.

Rais alikuwa akizungumza alikuwa mwenyekiti mwenza katika mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu pamoja na Rais wa Slovenia Nata’sa Pirc Musar, kuhusu jinsi ya kushirikisha Sayansi na uvumbuzi wa teknolojia pamoja na data katika hatua ya kuleta mabadiliko.

Awali kiongozi wa taifa alishiriki mkutano na ujumbe kutoka muungano wa milki za Kiarabu (UAE), katika Umoja wa Mataifa ukiongozwa na rais wa mkutano wa mazingira wa COP28 pamoja na waziri wa viwanda na teknolojia ya juu wa Miliki ya Kiarabu Sultan Ahmed Al Jaber.

Mwanzilishi wa microsoft Bill Gates, aliyekuwa meya wa New York Mike Bloomberg, rais wa chama cha kimataifa kuhusu uhifadhi wa mazingira  Razan Al Mubarak, walihudhuria mkutano huo.

Katika mkutano huo, Ruto alitoa wito wa mageuzi katika mfumo wa ufadhili wa kimataifa hasa namna ya ulipaji madeni pamoja na ustawishaji wa taasisi za fedha za kimataifa.

Alisema hatua hii itayawezesha mataifa ambayo hayajastawi kiuchumi kushiriki katika juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga pamoja na maendeleo.

Rais pia alishiriki katika mkutano kuhusu kilimo ulioongozwa kwa pamoja na shirika la kimataifa la Marekani kuhusu maendeleo USAID na wizara ya mambo ya nje ya Norwa

PCS
+ posts