Home Habari Kuu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaomba kikosi cha Umoja wa Mataifa kuanza...

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yaomba kikosi cha Umoja wa Mataifa kuanza kuondoka mwaka huu

0
kra

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi ametoa wito wa kuondolewa kwa haraka kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini mwake kuanza mwaka huu.

Aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumatano kwamba aliiagiza serikali yake kuanza mazungumzo na Umoja wa Mataifa ili kuleta “mwanzo wa hatua hii ya kujiondoa kutoka Disemba 2024 hadi Disemba 2023”.

kra

Alisema ujumbe huo – unaojulikana kwa kifupi kama Monusco – umeshindwa kuleta amani nchini humo licha ya kuwa huko kwa takriban miaka 25, na kuongeza kuwa ni “udanganyifu na usio na tija kuendelea kung’ang’ania” kikosi hicho ili kudumisha amani.

“Ni wakati wa nchi yetu kuchukua udhibiti kamili wa hatima yake na kuwa mstari wa mbele katika kuleta utulivu wake,” aliuambia mkutano huo New York.

Monusco – yenye wafanyakazi zaidi ya 16,000 – ni ujumbe wa pili kwa ukubwa wa Umoja wa Mataifa duniani na umezidi kutopendwa katika miaka ya hivi karibuni.

Umekosolewa kwa kushindwa katika dhamira yake ya kuleta utulivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hivyo kuzua maandamano hivi karibuni katika eneo hilo.

Mwaka jana, mwakilishi maalum wa Monusco wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliambia BBC kwamba ujumbe wa kulinda amani utatathminiwa kutokana na maandamano hayo mabaya, ambapo makumi ya watu waliuawa.

BBC
+ posts