Home Kimataifa Jamaa aliyekamatwa wakati wa maandamano aachiliwa na mahakama Nyahururu

Jamaa aliyekamatwa wakati wa maandamano aachiliwa na mahakama Nyahururu

0
kra

Mahakama ya Nyahururu imemwachilia huru jamaa kwa jina Robert Maina wa umri wa miaka 25, aliyekamatwa wakati wa maandamano Juni 25, 2024 na kukabiliwa na shtaka la kuchochea vurugu.

Kulingana na stakabadhi ya mashtaka, Robert alishtakiwa kwa kusema maneno “Ruto Must Go” tafsiri yake ikiwa “Ruto lazima aende” kinyume na sehemu ya 96 ya kanuni za adhabu.

kra

Mahakama ilielezewa kwamba jamaa huyo pamoja na wengine ambao hawakuwepo mahakamani walitamka maneno hayo katika kituo cha polisi cha Nyahururu, wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024, kabla ya kukamatwa.

Hakimu mkuu wa mahakama ya Nyahururu Evans Kiago hata hivyo alitupilia mbali mashtaka dhidi ya Robert kutokana na kile alichokitaja kuwa hatua ta upande wa mashtaka kukosa kudhibitisha mashttaka dhidi yake.