Home Habari Kuu Jaji Mkuu Martha Koome ampongeza mwenyekiti mpya wa LSK Faith Odhiambo

Jaji Mkuu Martha Koome ampongeza mwenyekiti mpya wa LSK Faith Odhiambo

Koome alisema kuchaguliwa kwa Bi. Odhiambo ni hatua kubwa ikizingatiwa kuwa yeye ni mwanamke wa pili kushikilia wadhifa huo katika historia ya taifa hili.

0
Mwenyekiti mpya wa LSK Faith Odhiambo.

Jaji Mkuu Martha Koome, amempongeza mwenyekiti mpya mteule wa chama cha mawakili nchini LSK Faith Odhiambo, pamoja na wanachama wengine wa baraza hilo, waliochaguliwa siku ya Alhamisi.

Koome alisema kuchaguliwa kwa Bi. Odhiambo ni hatua kubwa ikizingatiwa kuwa yeye ni mwanamke wa pili kushikilia wadhifa huo katika historia ya taifa hili.

“Hii ni hatua kubwa katika kuimarisha ujumuishaji katika mashirika ya kitaalam,” alisema Jaji huyo Mkuu, akisema anatazamia kushirikiana kwa karibu na mwenyekiti huyo mpya pamoja na baraza la chama hicho.

Wakati huo huo Koome ambaye pia ni Rais wa mahakama ya upeo hapa nchini, alimpongeza Omwanza Ombati, baada ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa kiume wa chama cha wanasheria nchini katika tume ya huduma za mahakama JSC.

Kupitia kwa taarifa, Jaji huyo Mkuu alisema idara ya mahakama na chama cha LSK, zimeshirikiana kwa pamoja kuhakikisha upatikanaji wa haki, kuimarisha mfumo wa utekelezaji haki na kuboresha uzingatiaji sheria hapa nchini.

Aliwapongeza wale wote waliowania nyadhifa mbali mbali katika uchaguzi huo kote nchini, kwa kudumisha amani wakati wa kipindi cha kampeni na uchaguzi.

Website | + posts