Home Michezo Jackson na Sifan wajiondoa mbio za mita 100 na 1500

Jackson na Sifan wajiondoa mbio za mita 100 na 1500

0
kra

Wanariadha Shericka Jackson wa Jamaica na  Sifan Hassan wa Uholanzi, wamejiondoa katika mbio za mita 100 na 1500 mtawalia katika makala ya mwaka huu ya Michezo ya Olimpiki jijini Paris, Ufaransa.

Jackson ambaye ni bingwa wa Dunia katika mita 200 alikuwa ametangaza kushiriki pia katika mbio za mita 100 mwaka huu, lakini amejiondoa huku nafasi yake ikitwaliwa na Shashalee Forbes.

kra

Jackson atashiriki mbio za mita 200 pekee.

Hassan kwa upande wake amejiondoa katika mbio za mita 1,500 na badala yake atatimka mbio za mita 5,000, 10,000 na marathoni.

Website | + posts