Home Habari Kuu Israel yakiri mamia ya raia wake wametekwa nyara na Hamas

Israel yakiri mamia ya raia wake wametekwa nyara na Hamas

0

Israel imetangaza kuwa mamia ya raia wake wametekwa nyara na kundi la wanamgambo la Hamas kufuatia shambulizi walilotekeleza juzi Jumamosi katika ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel Luteni Kanali Richard, akizungumza na wanahabari mapema leo Jumatatu, amesema raia wake walio matekani ni pamoja na wakongwe, watoto na familia huku akisisitiza uwezekano wa wanamgambo hao kuvuka mpaka na kuingia katika himaya ya Israel.

Jeshi la Israel limetangaza kudhibiti eneo la Gaza huku likiwa limetekeleza mashambulizi takriban 500 yanayokisiwa kufanywa katika maficho yya wanamgambo wa Hamas tangu juzi Jumamosi.

Raia zaidi ya 1,200 wa Israel wameuawa kufukia leo Jumatatu huku Wapalestina 500 wakiwa wameangamizwa katika makabiliano hayo.

Website | + posts