Home Kimataifa Israel yazitaka nchi kadhaa kuiwekea Iran vikwazo

Israel yazitaka nchi kadhaa kuiwekea Iran vikwazo

Waziri wa mambo ya nje, Israel Katz, ameziandikia makumi ya nchi akitaka vikwazo viwekewe mpango wa makombora wa Iran.

0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel anasema anaongoza “mashambulizi ya kidiplomasia dhidi ya Iran”, huku serikali ikizingatia jibu la kijeshi kwa shambulio la kombora na ndege zisizo na rubani dhidi yake mapema Jumapili.

Waziri wa mambo ya nje, Israel Katz, ameziandikia makumi ya nchi akitaka vikwazo viwekewe mpango wa makombora wa Iran.

“Leo asubuhi nilituma barua kwa nchi 32 na kuzungumza na mawaziri kadhaa wa mambo ya nje na watu mashuhuri ulimwenguni kuomba mradi wa makombora wa Iran uwekewe vikwazo,” Katz aliandika kwenye X.

Vile vile ametoa wito kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) kutangazwa kuwa shirika la kigaidi, “kama njia ya kuzuia na kuidhoofisha Iran”. Anaongeza: “Iran lazima idhibitiwe – kabla mambo hayajaenda mrama”

BBC
+ posts