Home Kimataifa Israel yawatambua raia wawili wa Tanzania walioshikwa mateka na Hamas

Israel yawatambua raia wawili wa Tanzania walioshikwa mateka na Hamas

Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga walikuwa nchini Israel kama sehemu ya programu ya mafunzo ya kilimo.

0
Raia wawili wa Tanzania walioshikwa mateka na Hamas.

Serikali ya Israel imethibitisha utambulisho wa watu wawili kutoka Tanzania, wanaoaminika kushikwa mateka na kundi la Hamas tangu shambulizi la tarehe saba Oktoba dhidi ya jamii za kusini mwa Israel, karibu na mpaka na Gaza.

Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga walikuwa nchini Israel kama sehemu ya programu ya mafunzo ya kilimo, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya mambo ya nje ya Israel.

“Walitekwa nyara na magaidi wa Hamas na wanazuiliwa mateka huko Gaza. Tafadhali ungana nasi kuwaombea warudi salama na mara moja.” Ilisema wizara hiyo.

Mollel na Mtenga walikuwa sehemu ya kundi la wanafunzi waliokuwa wakiishi Kibbutz Nahal Oz.

Walikuwa wametoweka tangu mashambulizi hayo, lakini Israel ilikuwa bado haijathibitisha utambulisho wao au kuripoti kilichowapata.

Tanzania ilisema Alhamisi kuwa inafahamu kuhusu wanafunzi wawili waliopotea ambao ni sehemu ya kundi la Watanzania 260 nchini Israel, lakini bado haijathibitisha walipo. Watanzania tisa waliokuwa Israel walirejea nyumbani Oktoba 18.

Website | + posts
BBC
+ posts