Home Habari Kuu Israel yatangaza vita na kuapa kulipiza kisasi Gaza

Israel yatangaza vita na kuapa kulipiza kisasi Gaza

0
kra

Hofu ya shambulizi katika ukanda wa Gaza inazidi kuongezeka baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuapa kugeuza eneo hilo kuwa mahame kama njia ya kujibu shambulizi baya zaidi ambalo limewahi kutekelezwa dhidi ya Israel kwa miongo mingi.

Matamshi yake yanajiri baada ya washambulizi kutoka Hamas ambayo inadhibiti Gaza kushambulia miji kadhaa ya Israel na kusababisha vifo vya watu wapatao 250 Jumamosi. Washambuliaji hao wanadaiwa kuondoka na mateka wanajeshi na raia wa kawaida.

kra

Hilo ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Israel tangu vita vya Yom Kippur miaka 50 iliyopita.

Jeshi la Israel lilijibu shambulizi hilo kwa kushambulia ukanda wa Gaza ambapo vifo zaidi ya 230 vilirekodiwa.

Wanajeshi wa Israel wanaripotiwa kuendelea kushambulia kwa mabomu eneo la Gaza na kupigana na wapiganaji wa Hamas katika eneo la kusini mwa Israel hadi Jumapili asubuhi.

Wapiganaji wa Hamas walielezea kwamba shambulizi lao dhidi ya Israel lilichochewa na hatua ya kutoheshimiwa kwa msikiti wa Al Aqsa na maovu ya Israel dhidi ya wapalestina katika muda wa miaka mingi.

Mohammed Deif, kamanda wa jeshi la Hamas alisema wakati umewadia kwa adui kuelewa kwamba hawezi kuendeleza maovu bila matokeo.

Netanyahu ametangaza hali ya vita nchini Israel, akawakusanya wanajeshi na kuahidi kupigana na Hamas hadi mwisho. Alishauri wapalestina walio kwenye ardhi ya Israel katika ukanda wa Gaza kuondoka mara moja.

Website | + posts