Home Kimataifa Israel yakana madai ya WHO kuhusu jeshi lake kutaka vifaa tiba kuondolewa

Israel yakana madai ya WHO kuhusu jeshi lake kutaka vifaa tiba kuondolewa

0

Israel imekanusha madai ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa limeamriwa na jeshi la Israeli kuondoa vifaa tiba katika bohari mbili za vifaa tiba Kusini mwa Gaza, kutokana na kile kilichotajwa kuwa “operesheni za ardhini zitasababisha visifae kwa matumizi”.

Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, alichapisha ujumbe kwenye mtandano wa X kuitaka Israel “kuondoa amri hiyo”.

Tangu wakati huo, idara ya kuratibu shughuli za serikali ya Israel imesema taarifa hizo si sahihi. Katika ujumbe wake idara hiyo imesema:

‘’Ukweli ni kwamba hatukukuelelekeza kuondoa vifaa tiba katika bohari na pia tuliweka bayana (na kwa maandishi ) kwa wawakilishi husika wa Umoja wa Mataifa.’’

‘’Kutoka kwa afisa wa Umoja wa Mataifa tulitarajia walau atoe taarifa sahihi.”

BBC
+ posts