Home Kimataifa Israel yaidhinisha mkataba wa kuachiliwa huru kwa mateka

Israel yaidhinisha mkataba wa kuachiliwa huru kwa mateka

Hatua hiyo iliafikiwa baada ya mkutano wa masaa kadhaa, japo maelezo zaidi kuhusu mkataba huo hayajatolewa.

0

Baraza la Mawaziri nchini Israel limepiga kura ya kuidhinisha mkataba wa kuachiliwa huru kwa maketa wa nchi hiyo wanaozuiliwa na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Hatua hiyo iliafikiwa baada ya mkutano wa saa kadhaa, japo maelezo zaidi kuhusu mkataba huo hayajatolewa.

Kabla ya mkutano huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alinukuliwa akisema kwamba Israel itaendeleza vita dhidi ya kundi la Hamas hata ikiwa mkataba wa kuachiliwa uhuru mateka utaafikiwa.

Israel ilianza kushambulia Gaza baada ya wanamgambo wa kundi la Hamas kuvuka mpaka na kuingia nchini Israel Okctoba 7, na kuwaua takribani watu 1,200 na kuwateka nyara wengine 200.

Taarifa ambayo pia ilichapishwa kupitia Kituo cha habari cha Palestina ambacho kimebeba taarifa rasmi za kundi la Hamas, ilisema mateka hao 50 wataachiliwa kwa kubadilishana na wanawake na watoto 150 wa Kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel.

Mkataba huo pia utaruhusu mamia ya malori yanayobeba misaada ya kibinadamu, vifaa vya matibabu na mafuta kuingia Gaza, kulingana na Hamas.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Israel ilisema haitashambulia wala kumkamata mtu yeyote huko Gaza wakati wa kipindi cha kusitishwa kwa mapigano.

Wizara ya Afya eneo la Gaza inayosimamiwa na kundi la Hamas, imesema zaidi ya watu 14,000 wakiwemo watoto 5,000 wameuawa kwenye mashambulizi ya Israel.

Website | + posts
BBC
+ posts