Home Kimataifa Israel yafanya mashambulizi kutoka angani, baharini na nchi kavu

Israel yafanya mashambulizi kutoka angani, baharini na nchi kavu

0

Jeshi la Israel linajihusisha na mashambulizi kutoka angani, baharini na nchi kavu dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

Mapigano ya leo asubuhi ni katika maeneo matano tofauti katika mji wa Gaza na kaskazini, ambapo operesheni ya ardhi ya Israel ilikuwa ikizidishwa hapo jana, na magharibi mwa Gaza ndiko kunako uvamizi mkubwa zaidi.

Hamas walitoa taarifa hapo jana kuwa wanapambana na jeshi la Israel kwa kutumia makombora ya vifaru.

Mashambulizi hayo ya anga yaliendelea usiku kucha hasa karibu na Hospitali ya Al-Quds karibu na Mji wa Gaza ambapo takriban watu 14,000 wamekita kambi katika hospitali hiyo.

Hospitali hiyo ilisema watu wanane waliunganishwa kwa mashine za kuokoa maisha na haikuwezekana kuzisogeza kwa sababu barabara nyingi karibu na hospitali hiyo zimeharibika, na mapigano makali na Hamas yalikuwa yakitokea umbali wa mita 500 kutoka hospitalini.

Israel inadhibiti barabara zote mbili – njia kuu za kutokea Gaza kaskazini na barabara ya pwani – kwa hivyo kutoka nje ya Gaza ni vigumu sana, watu wanahatarisha maisha yao kuondoka kuelekea kusini.

Theluthi mbili ya wakazi wanapata aina fulani ya misaada kutoka Misri kusini – takriban lori 300 na nyingine 100 zinatarajiwa leo – ingawa hali ya kibinadamu ni mbaya zaidi kwa wale walio kaskazini.

Takriban watu 700,000 huko Gaza hawana umeme, maji au mtandao.

BBC
+ posts