Home Habari Kuu Ireland, Uhispania na Norway kutambua Palestina kama taifa Mei 28

Ireland, Uhispania na Norway kutambua Palestina kama taifa Mei 28

0

Viongozi wa mataifa ya Uhispania, Norway na Ireland, wametangaza kutambua Palestina kama taifa kwa lengo la kuleta amani baina yake na Israel na mashariki ya kati Kwa ujumla, jambo ambalo limekumbatiwa na Hamas na utawala wa Gaza.

Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Store, ” Hakuwezi kuwa na amani mashariki ya kati pasipo na kutambua”.
Aliongeza kuwa, “katika vita ambapo makumi ya maelfu wamekufa na wengine kujeruhiwa, lazima tuweke hai njia ya kipekee ya suluhu la kisiasa baina ya Israel na Palestina; mataifa mawili yanayopakana na kuishia Kwa amani”, alisema Gahr Store.

Punde baada ya hayo, waziri mkuu wa Ireland Simon Harris alihutubia vyombo vya habari kuwa,”Leo hii Ireland, Norway na Uhispania zinatangaza kuitambua Palestina. kila mmoja wetu sasa atachukua hatua za Kitaifa zifaazo kufanikisha uamuzi huo”.

Kwa upande wake, waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez, alikashifu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuweka juhudi za kuwepo Kwa mataifa mawil kwenye hatari kubwa kupitia njia ya uchungu na uharibifu wa Gaza.

Kufuatia hatua hii, Israel imetangaza kuwaondoa mabalozi wake kwenye mataifa hayo Kwa mashauriano zaidi na kudai kuwa haitanyamaza kwani hatua hii italemaza harakati za mazungumzo ya amani yanayoendelea Cairo na pia kuwepo Kwa taifa hilo kutachangia ugaidi eneo hilo.

Kwa muda sasa, mataifa mengi yameshinikiza kuwepo Kwa taifa la Palestina kutokana na vita vinavyoendelea huko Gaza ambapo zaidi ya watu 35,000 wamekufa na wengine wengi. kujeruhiwa.