Home Habari Kuu Ipo haja ya kulinda maslahi ya watoto, asema Philomena Mwilu

Ipo haja ya kulinda maslahi ya watoto, asema Philomena Mwilu

Naibu huyo wa Jaji Mkuu alisema kesi zinazohusu watoto kudhulumiwa, hazikamilishwi kwa wakati, akitaja hatua hiyo kuwa uzembe wakati mtoto anaslia katika mfumo wa sheria kwa muda mrefu.

0
Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Naibu jaji mkuu Philomena Mwilu, ametoa wito kwa tasisi za sheria na uongozi, watu binafsi na jamii kwa jumla, kuhakikisha usalama na maslahi ya watoto yanalindwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mwezi wa huduma kwa watoto, Mwilu alisema takwimu kutoka idara ya mahakama, zinaashiria ongezeko la visa vya dhuluma dhidi ya watoto.

“Kile ninachohimiza ni tukomeshe dhuluma dhidi ya watoto. Tunapaswa kuacha tabia mbaya na kuonyesha adabu kwa watoto,”alisema naibu huyo Jaji Mkuu.

Alisema kesi zinazohusu watoto kudhulumiwa, hazikamilishwi kwa wakati, akitaja hatua hiyo kuwa uzembe wakati mtoto anaslia katika mfumo wa sheria kwa muda mrefu.

“Ucheleweshaji huo unasababishwa na sisi sote, na ni lazima tuwajibike kwa hali hii,”aliongeza Mwilu.

Mwezi wa huduma kwa mtoto wa mwaka huu unaogozwa na maudhui “Mfumo wa sheria kwa kuzingatia mtoto” ambao unalenga kupunguza mrundiko wa kesi zinazowahusu watoto, pamoja na kutoa uhamasisho kuhusu michakato ya maswala ya watoto kwa umma.

Aidha Mwilu aliwapongeza wadau wote katika mfumo wa sheria unaohusu watoto, kwa kujitolea kwao kwa kulinda maslahi, ulinzi na uimarishaji wa maisha na siku za usoni za watoto.

Website | + posts