Home Habari Kuu IG Koome awahakikishia maafisa wa idara ya mahakama usalama

IG Koome awahakikishia maafisa wa idara ya mahakama usalama

0
kra

Inspekta Mkuu wa Polisi, IG Japhet Koome ametoa hakikisho la usalama kwa maafisa wote wa idara ya mahakama kote nchini.

Koome ametoa taarifa hiyo kufuatia kuawa kwa Hakimu Mkuu Monica Kivuti Juni 13 mwaka huu na afisa wa polisi.

kra

Haya yanajiri baada ya Mahakimu na Majaji kutangaza mgomo wa siku tatu kulalamikia ukosefu wa usalama mahakamani.

Jaji Mkuu Martha Koome tayari ametangaza kusitishwa kwa huduma za mahakama Juni 18 ili kumwomboleza marehemu Kivuti.

Marehemu Kivuti alifyatuliwa risasi na polisi baada ya hakimu huyo kufutilia mbali dhamana ya mshukiwa mmoja wa kike aliyekabiliwa na kesi ya ulaghai wa pesa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here