Home Habari Kuu Inspekta Mkuu wa Polisi akutana na mtaalamu wa uchukuzi wa Benki ya...

Inspekta Mkuu wa Polisi akutana na mtaalamu wa uchukuzi wa Benki ya Dunia

0

Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome siku ya Jumatano alikutana na mtaalamu wa uchukuzi kutoka Benki ya Dunia katika makao makuu ya polisi jijini Nairobi.

Mazungumzo yao yaliangazia mikakati ya kukusanya takwimu kuhusu ajali za barabarani kwa lengo la kuimarisha usalama barabarani nchini Kenya.

Wakati wa mkutano huo, Koome alielezea kujitolea kwa huduma ya taifa ya polisi kuendeleza ushirikiano na benki hiyo pamoja na halmashauri ya uchukuzi na usalama barabarani, NTSA kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Kundi kutoka Benki ya Dunia iliongozwa na mchumi Sveta Milusheva.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Dkt. Duncan Kibogong kutoka NTSA.

Website | + posts