Home Biashara Indonesia kuisaidia Kenya kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia

Indonesia kuisaidia Kenya kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia

0

Wizara ya Biashara inasema Indonesia itaisaidia Kenya kuwa na mafuta ya kutosha ya kupikia kupitia kilimo cha mafuta ya mawese, yale ya alizeti na maharagwe ya soya kwa kiwango kikubwa. 

Indonesia ndio nchi inayozalisha mafuta ya mawese kwa wingi duniani.

Katika taarifa, wizara inasema ujumbe wa kampuni kinara za serikali na za kibinafsi za Indonesia unatarajiwa jijini Nairobi wiki ijayo.

Ujumbe wa Indonesia utaongozwa na Waziri wa Uratibu wa Mambo ya Majini na Uwekezaji Luhut Binsar Pandjaitan anayeratibu wizara saba katika serikali ya nchi hiyo.

Ujumbe huo utajadiliana na Rais William Ruto na Mawaziri Moses Kuria wa Biashara na Mithika Linturi wa Kilimo makubaliano ya ukuzaji wa kilimo cha mafuta ya kupikia kati ya nchi hizo.

Mazungumzo kati yao yataangazaia namna ya kuwasaidia wakulima katika kaunti za Lamu, Kwale, Tana River na Taita Taveta.

Kaunti zingine zinazolengwa ni Homa Bay, Migori, Kisumu na Busia.

Kenya kwa sasa inaagiza mafuta ghafi ya mawese yenye kima cha dola bilioni moja za Marekani kila mwaka kupitia kampuni tano ambazo ni Bidco, Kapa Oil, Pwani Oil, Menengai na Golden Africa.

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here