Home Michezo Inasikitisha! Xavi amlaumu Refa baada ya Barcelona Kukandwa na PSG

Inasikitisha! Xavi amlaumu Refa baada ya Barcelona Kukandwa na PSG

Barcelona walitwanga na PSG kwa jumla ya mabao 6-4

0

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandez amemuelekezea kidole cha lawama refa Istvan Kovacs’ raia wa Romania baada ya klabu yake kuondolewa na PSG kwa jumla ya mabao 6 kwa 4 (6-4) katika ligi ya klabu bingwa barani ulaya.

Barcelona ilipata pigo kunako dakika ya 29 baada ya beki wake wa Kati Ronald Araujo kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kosa la kumchezea visivyo Bradley Barcola katika eneo la hatari.

“Uamuzi wa kutoa kadi nyekundu uliharibu kabisa mchuano, kosa kama hilo halistahili kadi nyekundu, alisema Xavi.

‘Nilimwambia refa maamuzi yake yalikuwa mabaya, alikuwa ni janga, aliharibu mchezo’ Xavi aliongezea.

Shoka la refa halikumuacha peupe Xavi kwani alijipata pabaya kuelekea dakika za majeruhi alipoonyeshwa kadi nyekundu. Hii ni mara ya tatu kwa kocha huyo wa Barcelona kuonyeshwa kadi nyekundu msimu huu.

Barcelona walianza vizuri dhidi ya PSG katika dimba la Olympic wakitangulizwa kifua mbele na Raphinha lakini mkondo wa mchezo ulibadilika ghafla tu Barca walipopunguzwa na kuwa kumi uwanjani jambo ambalo Xavi anadhani halingekubalika kutendeka.

Baada ya Ronaldo Araujo kuonyesha kadi nyekundu, Barcelona ililazimika kumtoa kafari kinda Lamine Yamal ambaye alichangia kwa pasi saidizi iliyozaa matunda na kuwatanguliza Barca. Nafasi ya Lamine Yamal ikitwaliwa na Inigo Martinez kusudi kuziba nafasi ya Araujo.