Home Habari Kuu IGAD yawataka majenerali wa Sudan kujadiliana na kumaliza vita

IGAD yawataka majenerali wa Sudan kujadiliana na kumaliza vita

0

Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali, IGAD umetoa wito kwa pande zinazozozana nchini Sudan kukubali kusitisha vita na kuwataka majenerali wawili wanaohasamiana kushiriki mkutano wa ana kwa ana.

Hayo yaliafikiwa wakati wa Mkutano wa 42 Usiokuwa wa Kawada wa Viongozi Wakuu wa IGAD  uliofanyika mjini Entebbe nchini Uganda jana Alhamisi.

Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo. Wngine ni Marais Ismail Omar Guelleh (Djibouti), Yoweri Museveni (Uganda), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Hassan Sheikh Mohamud (Somalia).

Majenerali Abdel Fattah al-Burhan na Mohammed Hamdan Daglo wamekuwa wakizozana katika mzozo ambao ulianza Aprili 15, 2023 na kusababisha vifo vya maelfu ya raia wa Sudan.

Mamilioni ya raia wa nchi hiyo wamepoteza makazi na wengi wamekimbilia usalama katika nchi jirani kama vile Chad.

Jitihada za kuwapatanisha majenerali hao bado hazijazaa matunda.

Rais Ruto amekuwa mstari wa mbele kuwapatanisha, na amewahi kukutana nao jijini Nairobi nyakati tofauti katika jitihada za kumaliza mzozo huo.

 

Martin Mwanje & PCS
+ posts