Home Kimataifa IG Koome aagiza kufurushwa kwa majangili North Rift

IG Koome aagiza kufurushwa kwa majangili North Rift

Majangili waliojihami waliteketeza madarasa na afisi katika shule ya msingi ya Ngaratuko katika wadi ya Saimo Soi, kaunti ndogo ya Baringo kaskazini.

0
Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome.
kra

Inspekta Jenerali wa Polisi (IG) Japhet Koome, ameagiza kufurushwa kwa majangili katika eneo la North Rift, aliosema wanasambaratisha uchumi kwa kuharibu miundomsingi ya serikali.

Koome alitoa agizo, kufuatia kisa ambapo majangili waliojihami waliteketeza madarasa na afisi katika shule ya msingi ya Ngaratuko katika wadi ya Saimo Soi, kaunti ndogo ya Baringo kaskazini wakati wa siku kuu ya Pasaka..

kra

“Imetosha imetosha. Majangili hawa wamevuka mpaka na tutakabiliana nao bila huruma,” alisema Koome.

Koome alisema wahalifu hao pia waliharibu nyaya za umeme na mitambo ya umeme jua zinazomilikiwa na taasisi kadhaa katika kaunti ndogo za Baringo Kaskazini na Baringo kusini.

Mnamo siku ya Jumatatu, Koome aliagiza kupanuliwa kwa operesheni ya maliza uhalifu hadi kaunti za meru na Isiolo ambapo majangili wameelekea.

Website | + posts